Kufichuka kwa nyaraka za siri, changamoto kwa viongozi Ujerumani | Matukio ya Kisiasa | DW | 27.07.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Kufichuka kwa nyaraka za siri, changamoto kwa viongozi Ujerumani

Kufichuliwa kwa karibu nyaraka 92,000 za siri za jeshi la Marekani kuhusiana na hali nchini Afghanistan kunaleta sura ya wazi ya hali ya vita katika jimbo la Hindukush.

default

Wapiganaji wa Taliban ambao wanasemekana kuwa wameimarika zaidi hivi sasa pamoja na kuwa na silaha za kisasa zaidi.

Kufichuliwa kwa karibu nyaraka 92,000 za siri za jeshi la Marekani kuhusiana na hali nchini Afghanistan sura ya vita katika jimbo la Hundukush inaonekana wazi na pia kuleta hali ya kuvunjika moyo. Na pia kwasababu hali haionyeshi kimsingi mambo mapya, lakini baada ya kufichuka kwa nyaraka hizo za siri kuna hali mpya, ambayo ni mjadala wa kweli kuhusiana na kuwepo kwa majeshi ya Ujerumani nchini Afghanistan.

Nyaraka hizo za siri zilizowekwa wazi katika mtandao wa internet zinaleta vitu vitano vya kutambua, iwapo nyaraka zote ni za kweli. Ni lazima kufanya utaratibu huu wa kuzipunguza. Kwa kuwa hakuna anayejua , iwapo taarifa hizo, za idara ya upelelezi na hali iliyotolewa ni ya kweli na ya hivi sasa. Mtandao huo wa Wikileaks umeweka wazi , kuwa kwa kufichua siri hizo unataka kumalizwa kwa haraka kwa vita nchini Afghanistan. Hali hiyo iko karibu, kwamba kutokana na nyaraka hizo, kuwekwa kwa majeshi ya kimataifa kunakoonekana kuwa ni suala muhimu, kunapaswa kufikishwa mwisho.Mwishowe nyaraka 15,000 ambazo Wikileaks inazo hazijawekwa katika mtandao wa internet.

Mambo hayo matano kuhusu nyaraka hizo ni pamoja na vita dhidi ya ugaidi, Taliban na hali ya jeshi la kimataifa chini ya uongozi wa Marekani nchini Afghanistan kutostahili tena kuwapo. Wataliban wameimarika zaidi na wana silaha nzuri zaidi kuliko ilivyokuwa hapo kabla. Makomandoo maalum wanawatafuta viongozi wa ngazi za juu wa Taliban pamoja na viongozi wa makundi yanayoendesha biashara ya mihadarati, na hawa wanatakiwa kuuwawa ama kukamatwa. Maafisa wa Afghanistan , polisi na jeshi kwa sasa wameimarika zaidi kuliko ilivyofikiriwa hapo kabla, kutokana na kuwapo watu wasioweza kazi, wasaliti pamoja na mafisadi. Pia idara ya ujasusi ya Pakistan inawasaidia mno Wataliban.

Kwa kawaida watu walikwisha hisi hali kama hiyo, lakini hivi sasa inaleta hali ya kufadhaisha. Ujerumani ikiwa ni nchi ya tatu kuwa na ujumbe mkubwa nchini Afghanistan , imo katika hali ya kujiuliza, na pia kuwa na mjadala wa wazi hatimaye. Siri inabaki lakini bado katika upande wa wale wanaofahamu mengi ya ndani na pamoja na kila kilichowekwa wazi.

Ni vipi jeshi la Ujerumani linaweza kuchukua hatua za haraka kuhusiana na hali ya kitisho katika jimbo la Kunduz na kaskazini mwa Afghanistan. Lijiondoe haraka ama vikosi hivyo hatimaye sasa viimarishwe zaidi pamoja na kupewa silaha bora zaidi. Je ni kwamba serikali ya Ujerumani sasa itakiri kuwa mkakati wa hivi sasa wa ujenzi mpya wa miradi ya kijamii, ambayo raia wa nchi hiyo hadi sasa wameifurahia , imekuwa ni kazi bure?. Je lengo la vita hivi ambalo ndio kiini cha kazi yote hiyo inayofanyika , la kuwamaliza Wataliban na magaidi litafupishwa? Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Guido Westerwelle ambaye alionekana kuwa na matumaini makubwa haonekani tena kuwa na hali ya kujua la kufanya. Ni lazima lakini alieleze wazi bunge kwamba ni ndoto kufikiria kuwa Afghanistan inaweza kuimarishwa usalama wake ifikapo mwaka 2014 na kuachwa ikiwa katika hali ya utulivu.

Mwandishi : Bernd Riegert / ZR / Sekione Kitojo

Mhariri : Josephat Charo.

 • Tarehe 27.07.2010
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/OVWm
 • Tarehe 27.07.2010
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/OVWm
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com