1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KUFA: Moqtada al-Sadr amejitokeza hadharani Iraq

25 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CByM

Kiongozi wa Kishia mwenye msimamo mkali,Moqtada al-Sadr amejitokeza hadharani nchini Iraq kwa mara ya kwanza,baada ya miezi kadhaa.Maafisa wa Kimarekani hapo awali walisema,kiongozi huyo alikimbilia Iran mwezi wa Januari,kabla ya vikosi vya Marekani kuimarisha operesheni zake katika mji mkuu wa Iraq,Baghdad.Habari hiyo haijawahi kuthibitishwa.Moqtada al-Sadr,akizingirwa na walinzi na wasaidizi wake,alihudhuria Sala ya Ijumaa mjini Kufa,mashariki mwa Iraq.Sadr ni kiongozi wa kundi la wanamgambo wa madhehebu ya Kishia liitwalo,Jeshi la Mehdi ambalo hulaumiwa kuhusika na baadhi ya mauaji ya kimadhehebu nchini Iraq. Alipokuwa mafichoni,Sadr aliwatoa mawaziri sita wanaomuunga mkono,kutoka serikali ya Iraq,katika juhudi ya kumshinikiza Waziri Mkuu Nouri al Maliki kupanga tarehe ya kuondosha vikosi vya Marekani nchini Iraq.