Kosovo yatazamiwa kutangaza uhuru wake Jumapili | Habari za Ulimwengu | DW | 16.02.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Kosovo yatazamiwa kutangaza uhuru wake Jumapili

Umoja wa Ulaya waifungulia njia Kovoso baada ya kuidhinisha kikosi chake maalum kwenda huko

PRISTINA

Umoja wa Ulaya umeidhinisha kikosi cha polisi wa kiraia na ujumbe wa kisheria kusaidia kuweka utawala wa kisheria katika jimbo la Kosovo ambalo limejiandaa kutangaza uhuru wake kutoka kwa Serbia.

Ujumbe huo mzito wa askari 2000 wa Umoja wa Ulaya utaanza kupelekwa katika eneo hilo kuanzia wiki ijayo.Marekani na zaidi nchi za Ulaya zimejiandaa kuutambua uhuru wa jimbo la Kosovo kwa haraka lakini Serbia na Urussi zinapinga vikali hatua hiyo ambayo inatarajiwa kuchukuliwa hapo kesho.Waziri mkuu wa jimbo la Kosovo amewahakikishia waliowachache katika jimbo hilo kwamba utawala wake hautawabagua.Hatua ya Umoja wa Ulaya imekuja baada ya hapo jana kuapishwa kuingia madarakani rais Boris Tadic wa Serbia anaunga mkono nchi za magharibi.Ujumbe wa Umoja wa Ulaya utakaokwenda Kosovo unajumuisha maafisa wa forodha,majaji na waendesha mashtaka ambao watahusika katika kuzuia uvunjwaji wa haki za binadamu na kuhakikisha taasisi dhaifu katika jimbo hilo la Kosovo zinaendesha shughuli zake kwa njia ya uhuru bila ya kuingiliwa kisiasa.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com