Korea Kusini kuijibu Korea Kaskazini kwa makombora | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 24.11.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Korea Kusini kuijibu Korea Kaskazini kwa makombora

Hatua hiyo inatokana na shambulio lililofanywa na Korea Kaskazini katika kisiwa cha Korea Kusini.

default

Wa-Korea Kusini wakiomboleza vifo vya wanajeshi wawili waliouawa katika shambulio la Korea Kaskazini.

Korea Kusini imesema itaishambulia Korea Kaskazini kwa makombora, iwapo nchi hiyo itachukua hatua zaidi za kiuchokozi. Hatua hiyo inatokana na shambulio lililofanywa na Korea Kaskazini katika kisiwa cha Korea Kusini mapema jana.

Pande hizo mbili zilifyatuliana risasi kwa muda wa saa moja, ikiwa ni moja kati ya mashambulio mabaya kabisa kutokea baina ya nchi hizo mbili kwa karibu miaka 60 iliyopita. Kiasi wanajeshi wawili wa Korea Kusini waliuawa huku wengine kadhaa wakiwa wamejeruhiwa. Rais wa Korea Kusini, Lee Myung-bak amesema shambulio hilo linahitaji kujibiwa kwa nguvu.

Shambulio hilo limeshutumiwa vikali na jumuiya ya kimataifa. Rais Barack Obama wa Marekani amekiita kitendo hicho kama cha ''uchochezi na kuchukiza'' na kwamba Marekani itasimama katika kumlinda mshirika wake huyo. Aidha, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon amezitaka pande zote mbili kujizuia na mazoezi.

 • Tarehe 24.11.2010
 • Mwandishi Kabogo Grace Patricia
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/QGbM
 • Tarehe 24.11.2010
 • Mwandishi Kabogo Grace Patricia
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/QGbM
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com