Korea Kaskazini yarusha makombora mawili ya masafa mafupi | Matukio ya Kisiasa | DW | 25.07.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Korea Kaskazini yarusha makombora mawili ya masafa mafupi

Jeshi la Korea Kusini limesema Korea Kaskazini imerusha makombora mawili ya masafa mafupi kutoka eneo la Mashariki ya Pwani yake.

Makombora hayo yaliozinduliwa katika mji wa Pwani wa Wonsan, yaliruka umbali wa kilomita 430 juu ya usawa wa bahari na kufikia urefu wa kilomita 50 kabla ya kuanguka. Haya ni kulingana na afisa mkuu wa wizara ya ulinzi ya Korea Kusini aliyezungumza na shirika la habari la Reuters. Korea Kaskazini hukasirishwa na majaribio ya kijeshi yaliopangwa na Marekani na Korea Kusini ambayo inasema zinajitayarisha kuiingilia.

Wadadisi wamesema jaribio hilo la makombora huenda limefanyika kama onyo kwa Marekani. Kutokana na hatua hiyo ya Korea Kaskazini kurusha makombora hayo, waziri wa ulinzi wa Korea Kusini Choi Hyun. Soo amesema

Kurushwa kwa makombora hayo, kunatilia shaka juhudi za kuanzisha upya majadiliano kuhusu nyuklia ya Korea Kaskazini, baada ya rais Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un kukutana katika eneo lisilokuwa na shughuli za kijeshi kati ya mataifa hayo mawili ya Korea.

Haya yamejiri mnamo wakati wengi nchini Marekani wameelekeza nadhari kwenye ushahidi uliotolewa bungeni na Robert Muller, mchunguzi maalumu wa zamani, kuhusu uchunguzi wake uliodumu kwa miaka miwili juu ya uingiliaji wa urusi katika uchaguzi wa Marekani. Siku moja kabla ya hayo, mshauri wa kitaifa wa masuala ya usalama John Bolton aliondoka Korea Kusini baada ya kukubaliana na maafisa wakuu wa serikali ya nchi hiyo, kushirikiana katika kufikia lengo la Korea Kaskazini kusitisha matumizi ya kinyuklia.

 

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com