1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kaskazini

Korea Kaskazini yaonyesha silaha zake katika gwaride

9 Februari 2023

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un aliongoza jana gwaride kubwa la kijeshi ambalo liliadhimisha kumbukumbu ya miaka 75 ya kuanzishwa kwa jeshi.

https://p.dw.com/p/4NHBh
Nordkorea Pjöngjang | Militärparade zum 75. Gründungstag der Streitkräfte
Picha: KCNA/REUTERS

Kwa muda mrefu, Korea Kaskazini imekuwa ikitafuta mbinu za kutengeneza makombora ya nyuklia ambayo itakuwa vigumu kuyagundua na kuyaharibu.

Waangalizi wamekuwa wakifuatilia kwa karibu gwaride hizo za kijeshi ili kufahamu maendeleo ya nyuklia ya serikali ya Kim.

Korea Kaskazini imefanya gwaride nne za kijeshi nyakati za usiku katika miaka ya hivi karibuni, na imeapa kupanua na kuimarisha mazoezi ya kijeshi ili kuhakikisha kuwa wako tayari kwa vita.

Wachambuzi wanasema silaha zilizoonyeshwa katika gwaride la hapo jana, ni changamoto kubwa kwa Marekani.