Korea Kaskazini yajadiliwa. | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 07.12.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Korea Kaskazini yajadiliwa.

Mawaziri wa mambo ya nchio za nje wa Marekani, Japan na Korea kusini wamekutana jana kuijadili Korea kaskazini.

default

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani Hillary Rodham Clinton.

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani Hillary Clinton amefungua mkutano aliouita kuwa ni muhimu na mawaziri wenziye kutoka katika nchi za Japan na Korea kusini kujadili vitendo vya uchokozi vilivyofanywa na Korea kaskazini hivi karibuni.

Viongozi hao pia wameishinikiza China na Urusi kutuliza hali ya wasiwasi iliyoko katika eneo la rasi, ambalo China imeonya kuwa itashindikana kuzuilika iwapo halitadhibitiwa ipasavyo.

Novemba 23 mwaka huu, Korea kaskazini ilikishambulia kisiwa cha Yeonpyeong kilichopo Korea kusini, ikiituhumu Seol kwamba inajaribu kuanza tena vita kwa kutumia ujanja mpya.

Südkorea Insel Yeonpyeong Beschuss durch Nordkorea

Kisiwa cha Yeonpyeong, cha Korea kusini kilichoko mpakani na Korea kaskazini ambacho kimeshambuliwa.

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu itachunguza kama shambulio hilo la Korea kuskazini dhidi ya kusini ni uhalifu wa kivita.

 • Tarehe 07.12.2010
 • Mwandishi Halima Nyanza
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/QRB5
 • Tarehe 07.12.2010
 • Mwandishi Halima Nyanza
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/QRB5

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com