1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Korea Kaskazini yafyatua tena makombora

Saleh Mwanamilongo
14 Aprili 2020

Korea ya kaskazini imefanya majaribio mapya ya makombora kuelekea bahari ya Japan. Taarifa hii imetolewa na Korea Kusini na kusema kwamba makombora hayo yalikuwa ni ya masafa mafupi.

https://p.dw.com/p/3aryt
Nord Korea | Rede von Kim Jong Un
Picha: Reuters/KCNA

Korea ya kaskazini imefanya majaribio mapya ya makombora kwenye bahari ya Japan. Jeshi la Korea ya kusini ambalo limetoa taarifa hiyo limeeleza kwamba makombora hayo ya masafa mafupi yamefyatuliwa Korea ya kaskazini imefanya majaribio mapya ya makombora kwenye bahari ya Japan 

Taarifa ya jeshi la Korea Kusini inaelezea kwamba makombora hayo ya masafa mafupi yalifyatuliwa toka mji wa Munchon, mashariki mwa Korea Kaskazini.

Majaribio hayo yamefanyika mkesha wa maadhimisho ya miaka 108 ya Kim II Sung, muanzilishi wa taifa la Korea Kaskazini na babu wa rais wa sasa Kim Jong Un, lakini pia ikiwa ni mkesha wa uchaguzi wa bunge kwenye nchi jirani ya Korea Kusini.

Majaribio hayo ya makombora yamekuja wakati shinikizo kutoka kwa mataifa tajiri zaidi duniani dhidi ya Korea KaskaziniKorea Kaskazini yasema itazindua silaha mpya ya kimkakati likiwa limepungua kutokana na mripuko wa virusi vya corona. Korea Kaskazini inadai haijavamiwa na janga hilo hadi sasa.

Nordkorea | Raketentest
Korea Kaskazini imeendelea kufanya majaribio ya makombora kila wakati, licha ya shinikizo la kuachana na majaribio hayoPicha: picture-alliance/dpa/KCNA

Miaka ya hivi karibuni Korea ya Kaskazini, nchi yenye silaha za kinyuklia, ilifanya majaribio kadhaa ya makombora ya masafa marefu. Nchi hiyo inasisitiza pia kwamba makombora yake yana uwezo wa kuyafikia maeneo mengi ulimwenguni, ikiwemo Marekani.

Jeshi la Korea Kusini linaelezea kwamba majaribio ya Jumanne ya makombora yalielekezwa kwenye bahari ya Mashariki.

Korea Kusini na idara za kiusalama za Marekani wanachunguza kwa karibu masuala yanayohusiana na majaribio hayo ya makombora, inaelezea taarifa ya jeshi la Korea Kusini.

Korea ya Kaskazini iliwekewa vikwazo na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa ili kuilazimisha kusitisha mipango yake ya kutengeneza makombora na silaha za kinyuklia.

Majaribio ya makombora ya masafa mafupi hayakiuki maazimio ya Umoja wa Mataifa, kwa mujibu wa wataalamu wa masuala ya kijeshi wa umoja huo.

Nordkorea | Neue Raketentests
Picha hii inawaonyesha wanajeshi wa vikosi vya Korea Kaskazini wakiwa kwenye mmoja wa mtambo wa kijilindaPicha: picture-alliance/Yonhap

Soma Zaidi: Korea Kaskazini imesema imefanya "jaribio muhimu sana"

Miaka ya nyuma Korea Kaskazini ilifanya majaribio mengi ya makombora ya masafa marefu. Mwaka 2017, Pyong Yang ilijisifu kufanikiwa katika majaribio yake ya makombora ya baharini ambayo yana uwezo wa kubomoa jengo lolote.

Majaribio hayo yalifanyika kwenye maeneo ya bahari ambako meli za jisheri za Marekani zilifanya mazoezi yake ya kijeshi wiki moja kabla.

Makombora hayo yalirushwa kilomita mia mbili kabla ya kusambaratika kwenye bahari. Wataalamu walithibitisha kwamba jaribio hilo ni mafanikio makubwa kwa Korea Kaskazini, ukilinganisha na jaribio la mwaka 2015 ambalo makombora hayo yalirushwa umbali wa kilomita 150.

Kim Jon Un na rais wa Marekani Donald Trump walitupiana maneno makali na kutishia makabiliano ya kinyuklia kabla ya kufanya mkutano wa kihistoria. Hata hivyo mazungumzo yao ya Februari 2019 mjini Hanoi hadi sasa hayajapiga hatua.

Mashirika.