Korea kaskazini yaendeleza vitisho | Matukio ya Kisiasa | DW | 03.04.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Korea kaskazini yaendeleza vitisho

Hali ya wasiwasi imezidi katika rasi ya Korea baada ya Korea Kaskazini kufunga maeneo muhimu yanayounganisha eneo la viwanda na Korea Kusini, huku Urusi na China zikiitaka Korea kusitisha zoezi hilo.

epa03633724 A picture released by the North Korean Central News Agency (KCNA) on 20 March 2013 saying the North Korean army is completely ready to fight against South Korea and the United States. North Korea threatened to attack US bases in Japan and on Guam 21 March 2013 in reaction to flights by US B-52 bombers in South Korea during joint manoeuvres, while the Stalinist state also activated air raid alerts. The North Korean army's command accused the United States of preparing for a nuclear war in its ongoing exercises with the South Korean military. EPA/KCNA SOUTH KOREA OUT EDITORIAL USE ONLY/NO SALES +++(c) dpa - Bildfunk+++

Nordkorea erklärt Kriegszustand

Wasiwasi huo unakuja baada ya Korea Kaskazini kufunga mipaka yake ya kijeshi iliyopo umbali wa kilomita 11 upande wa Kaskazini, na kuzuia zaidi ya Wafanyakazi 861 wa Korea Kusini na wafanyakazi 53,000 wa Korea Kaskazini waliokuwa wanafanya kazi katika eneo la viwanda la Kaesong.

Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong Un

Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong Un

Kufuatia hali hiyo waziri wa ulinzi wa Korea Kusini, ametishia kuwa serikali yake itafanya kila liwezekanalo hata kama ni kutumia jeshi ili kulinda usalama wa raia wa Korea Kusini waliokuwa wakifanya kazi katika eneo hilo ambalo linatumiwa na Korea mbili.

Meneja wa moja ya viwanda katika eneo hilo, Lee Jae-Young, akiongea na Shirika la habari la AFP amesema, hatua hiyo imeathiri mzunguko wa biashara na uzalishaji baada ya malighafi nyingi za viwanda hivyo zinazosafirishwa kwa meli kwenda eneo la Kaesong kwa ajili ya uzalishaji, kukwama.

Jamii ya Kimataifa yatoa maoni

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani, Guido Westerwelle, amezitaka pande mbili kuacha uchokozi na kukaa pamoja huku Westerwelle akiikosoa vibaya Korea Kaskazini kwa kutangaza pia kuendelea kutengeneza silaha za nyuklia, na kuwataka wasafiri Korea Kusini kutoingia Korea Kaskazini kwa sasa.

Kwa upande wake naibu Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Urusi, Igor Morgulov, amesema kuwa kuna haja ya kuchukua tahadhari kwani kosa dogo la kibinadamu, linaweza kusababisha vita ambavyo havitaweza kusimamishwa, na kuwa hatua ya Korea Kaskazini si tu itatia dosari uhusiano wa kidiplomasia kati ya Korea mbili, bali utachafua sura ya Korea Kaskazini katika jamii ya kimataifa.

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani

Ufaransa nayo pia imeitaka China ambayo ina nguvu ya kuishawishi Korea Kaskazini, iingilie kati mgogoro wa kijeshi unaotokota katika rasi ya Korea.

China ambayo imekuwa na misimamo ya kindumakuwili ambayo ilikuwa rafiki wa karibu wa Korea Kaskazini kwa miongo kadhaa na mshirika wa kibiashara, imefungua kinywa na kuitaka Korea Kaskazini kumaliza mgogoro uliopo Rasi ya Korea.

Uchokozi huo ulianza kushuhudiwa katika rasi ya Korea tokea Korea Kaskazini ilipofanya jaribio lake la mwanzo mwezi Desemba mwaka jana la kurusha kombora la masafa marefu na kufanya jaribio lake la tatu la Nyuklia mwezi Februari mwaka huu, matukio ambayo yalisababisha iwekewe vikwazo na Umoja wa mataifa.

Mwandisahi: Hashim Gulana/AP/AFP/DPAA

Mhariri: Josephat Charo

DW inapendekeza

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com