1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroKorea Kaskazini

Kim Jong Un aahidi kuendelea kuisaidia Urusi kivita

30 Novemba 2024

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amesema ataendelea kuisaidia Urusi katika vita vyake dhidi ya Ukraine.

https://p.dw.com/p/4nbMW
Rais Vladimir Putin azuru Korea Kaskazini
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un akiwa na Rais wa Urusi Vladimir Putin. Kim ameahidi kuendelea kuisaidia Urusi kupambana na UkrainePicha: Vladimir Smirnov/POOL/TASS/dpa/picture alliance

Kim ametoa hakikisho hilo mbele ya Waziri wa Ulinzi wa Urusi Andrei Belusov, anayezuru Pyongyang.

Kim amenukuliwa na vyombo vya habari mapema leo akisema Korea Kaskazini itaunga mkono sera ya Urusi ya kujilinda na kutetea uhuru wake dhidi ya hatua za kibabe za mabeberu 

Kim ameikosoa hatua ya mataifa ya magharibi yakiongozwa na Marekani kwa kuiruhusu Ukraine kuyashambulia maeneo ya Urusi kwa kutumia silaha zao za masafa marefu, na kuitaja kama uingiliaji wa moja kwa moja kwenye mzozo huo, ikimaanisha Urusi inatumia haki yake ya kujilinda na kuhakikisha vikosi vya adui vinalipa gharama.