1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Kombora la Urusi laua watu 3 huko Zaporizhzhia

2 Machi 2023

Polisi nchini Ukraine imefahamisha kuwa watu watatu wameuawa na wengine wanne kujeruhiwa baada ya Urusi kufyatua kombora katika jengo la ghorofa kusini mwa nchi hiyo katika mji wa Zaporizhzhia.

https://p.dw.com/p/4O9Ru
Ukraine Krieg Front Horlivka
Picha: Oleksandr Ratushniak/REUTERS

Idara ya serikali ya Ukraine inayotoa huduma ya dharura imebaini katika ripoti kuwa watu 11 wameokolewa kutoka sehemu ya jengo lililoporomoka.

Uvamizi wa Urusi nchini Ukraine unatazamiwa kuwa mada kuu katika mkutano wa Mawaziri wa mambo ya nje wa G20 unaofanyika mjini New Delhi.

Wajumbe wa Ulaya na Marekani wamesisitiza kuwa wataiwajibisha Urusi kwa mzozo huo huku Ujerumani ikisema kuwa ingetumia mkutano huo kukabiliana na "propaganda" za Urusi.