Kombe la klabu bingwa uwanjani | Michezo | DW | 29.02.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Kombe la klabu bingwa uwanjani

Mwishoni mwa wiki hii kombe la klabu bingwa barani Afrika larudi uwanjani huku Manchester ikiahidi kuipiku Arsenal.

default

Kevin Kuranyi-jogoo la Schalke.

Kinyan’ganyiro cha kombe la klabu bingwa barani Afrika kinarudi uwanjani mwishoni mwa wiki hii huku timu ya wanajeshi wa Gabon FC 105 ikila kiapo kutamba mbele ya mabingwa wa zamani Hearts of Oak ya Ghana. Sawa na Hearts of Oak ,mabingwa wengine Union Douala wanakaribia pia kuzikwa mwishoni mwa wiki hii.

Katika Bundesliga,shoka lasemekana kumeta-meta kuwafyeka makochja 2 maarufu-Mirko Slomka wa Schalke 04 na Armin Veh wa mabingwa Stuttgart.Kisa nini ?

Subiri utasikia.

Katika Premier League-Manchester United yatumai kuipiku Arsenal na mwishoe kutetea taji lake la ubingwa.

Mabingwa wa wili wa zamani wa kombe la klabu bingwa barani afrika-Union douala ya Kamerun na Hearts of Oak ya Ghana tayari wamechimbiwa kaburi na ikiwa hawatachunga mwishoni mwa wiki hii watazikwa na kuaibishwa wakitolewa duru ya kwanza tu ya kinyan’ganyiro hiki.Timu zote hizo mbili zinapaswa kupania kufuta madhambi ya duru ya kwanza ya mpambano wa pili zikicheza mara hii nyumbani ama sivyo, wapewe buriani.

Jumla ya mapambano 23 yanachezwa mwishoni mwa wiki hii .Hearts of Oak waliotwaa kombe hili mara ya mwisho miaka 8 iliopita walikandikwa mabao 3-0 mjini Libreville, na wanajeshi wa FC 105 wa Gabon wameapa kuwapiga kumbo kabisa kwao mjini Accra.Jumapili iliopita Hearts of oak ilizabwa mabao 2:0 na Real Tamale United.

Wenazo Union Douala huko Kamerun wanabidi kufuta mabao 3-1 waliochapwa na ASKO kara ya Togo ,lakini kikosi chao hikionershi kimekomaa zahama za watogo.Kwani kiko mbali na ile timu yao iliotoroka na kombe 1979 hadi douala.

Mabingwa mara 5 Zamalek ya Misri wanatamba nyumbani baada ya kuondoka kigali katika duru ya kwanza kwa ushindi wa mabao 2:1 dhidi ya APR FC .Wenzao wa Tunisia Club Africain pia wana matumaini mazuri wakikutana tena na Saloum –wanagenzi wa Senegal .

Kuna timu 10 zinazocheza nyumbani mwishoni mwa wiki hii na ni pamoja na mabingwa wa afrika kusini –Mamelodi Sundowns ambao licha ya kuilaza Miembeni ya Zanzibar huko Amani,walimtimua kocha wao Gordon Igesund kutokana na kutocheza uzuri katika Ligi ya nyumbani.

Ama katika Ligi mashuhuri za Ulaya ,macho yanakodolewa mpambano wa leo kati ya viongozi wa ligi Bayern Munich na mahasimu wao wa karibuni Schalke 04.Ingawa Schalke ilimudu ushindi wa bao 1:0 nyumbani katika dhidi ya FC porto ya ureno katika champions League-kombe la klabu bingwa barani ulaya hivi majuzi iliteleza mara 2 katika patashika za bundesliga .

Leo Schalke wanacheza nyumbani lakini wanaelewa wana kibarua kigumu mbele ya Bayern Munich inayotaka kupanua mwanya wake kileleni kati yake na werder Bremen.

Kuna wanaodai hatima ya kocha wa schalke Mirko Slomka inategemea firimbi ya mwisho itakavyolia ya mpambano huu.baada ya kulazwa na Wolfsburg mabao 2-1,Schalke ilikumtwa bao 1-0 na bayer Leverkusen.Kwa mashabiki na uongozi wa Schalke,maji yamezidi unga.

Hatima ya Armin Veh wa mabingwa Stuttgart pia imnazungumzwa .Stuttgart ina miadi leo huko mashariki mwa Ujerumani na Energie Cottbus na mambo yakienda kombo nisingependa kuagua iwapo Armin Veh ataweza kulikwepa shoka la kumfyeka au la.

Manchester United ina yakini kwamba mwishoe itaziba mwanya wake na Arsenal London na kuipiku ili kutetea taji lake la ubingwa msimu huu.

Uongozi wa Arsenal umepunguzwa hadi point 3 huku zikisalia duru 11 za Ligi hii baada ya Arsenal kumudu suluhu tu ya mabao 2:2 na Birmingham wakati Manchester united iliirarua mapnde 2 Newcastle kwa mabao 5-1.

Real Madrid ya Spain lazima izuwie kuteremka mlima na kuepuka kupitwa na mahasimu wao FC Barcelona katika Ligi ya Spian.Uongozi wa Real kileleni kati yake na Barcelona umepungua hadi pointi 2.Madrid ina pointi 56 kwa 54 za Barcelona inayotamba sasa tena na jogoo lake Samuel eto’0 wa Kamerun.

Katika Serie A, Ligi ya Itali Inter Milan inajikokota sasa kutia mfukoni taji lake la 3 mfululizo.As Roma iliopo nafasi ya pili ya ngazi ya Ligi ilitoka sare bao 1-1 na Inter Milan juzi jumatano.Roma ina miadi na Parma na Juventtus iliopo nafasi ya 3 inacheza Fiorentina.AC Milan imerefusha mkataba wa mwanasoka bora wa mwaka wa dunia Kaka wa Brazil hadi 2013.Ac Milan inacheza na Lazio.

Katika Ligi ya Ufaransa, viongozi mashuhuri wa kispoti nchini Ufaransa ,wameungana kupiga vita ukabila katika dimba la Ufaransa-makamo-bingwa wa dunia. Miongoni mwao ni mfaransa rais wa UEFA Michel Platini,waziri wa michezo Bernard Laporte na rais wa Ligi ya Ufaransa Frederic Thiriez.Mwishoni mwa wiki iliopita –vijana-manazi-mambo-leo walitia dosari Ligi hiyo kwa kutoa saluti za kinazi huko Lyon.

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com