KOMBE LA KLABU BINGWA AFRIKA | Michezo | DW | 02.04.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

KOMBE LA KLABU BINGWA AFRIKA

Munich na Wolfsburg uwanjani leo:

default

Luca Toni.

Katika Kinyanganyiro cha Kombe la klabu bingwa barani Afrika, Young Africans ya Tanzania inajaribu leo kufuta mabao 3 ya mabingwa wa Afrika Al Ahly mjini Dar-es-salaam-wataweza ?Macho yakodolewa mpambano wa bundesliga leo kati ya mabingwa Bayern Munich na Wolłfsburg-zote mbili zikiwa na pointi sawa 48-pointi 1 nyuma ya viongozi wa Ligi Hertha Berlin.

FIFA imepokea maombi ya tiketi milioni 1.6 kwa kombe lijalo la dunia 2010 nchini Afrika Kusini na Ivory Coast, imeapa kuwaadhibu wale waliosababisha msiba wa jumapili iliopita pale mashabiki 22 walipofariki dunia Malawi ilipokandikw amabao 5 na Tembo wa Corte d-Iviore:

Macho yanakodolewa viwanja mbali mbali ijumamosi jioni kwa changamoto za Kombe la klabu bingwa barani Afrika huku mabingwa watetezi Al Ahly ya Misri ,waliwasili tangu juzi mjini Dar-es-salaam kwa miadi yao ya jioni hii na mabingwa wa Tanzania -Young Africans. Yanga iliwaonea mabingwa wa Comoro ilipowajazia kapu lao mabao 14 kabla hawakwenda Cairo.Leo basi Yanga wana kibarua kigumu cha kufuta mabao 3:0 waliopewa zawadi walipotembelea Cairo,wiki mbili zilizopita.

Wakati Young Afrika inatimiza miadi yake na mabingwa Al Ahly, majirani zao wa Afrika Mashariki Kampala City Council walifunga safari kwenda Afrika Kusini kutetea ushindi wao wa nyumbani wa mabao 2:1.

Djoliba ya Mali inacheza nyumbani na Club Africain ya Tunisia.Mizinga ya Canon Yaounde imelengwa leo kwa Primeiro Agosto ya Angola ikitegemea kupanua zaidi ushindi wake wa kwanza wa baso 1:0.Mjini harare,Mangasport ya Gambia inakumbana na Contonsport Garoua ya Kamerun wakati Monomotapa ya Zimbabwe inacheza na Ajax capetwon ya Afrika kusini.ZESCO UTD ya Zambia ina changamoto na Africa Sports ya Corte d-Iviore mjini Ndola.

Al Merrekh ya Sudan inachuana na Al Ittihad ya Libya. TP Mazembe ya jamhuri ya Kidemokrasi ya kongo, inapambana na Petro Atletico ya Angola. Washindi wa duru hii wagtacheza katika duru ijayo ya kuanza hasa kuania Kombe hilo.

Nje ya kombe la klabu bingwa barani Afrika, FIFA-shirikisho la kabumbu ulimwenguni,limeamrisha uchunguzi kufanywa juu ya ajali iliozuka uwanjani mjini Abidjan,Ivory Coast,ijumapili iliopita pale mashabiki kiasi ya 22 walipofariki dunia katika vurumai iliozuka uwanjani.Mashabiki wengine 132 walijeruhiwa -hii ilipelekea FIFA kuomba timu kadhaa zilizoteremka uwanjani Jumatano wiki hii kuania tiketi za Kombe lijalo la dunia ,kuomboleza uwanjani wenzao marehemu.FIFA imeliomba Shirikisho la mpira la Ivory Coast kulipatia ripoti juu ya mkondo wa mambo uliopelłekea vifo hivyo uwanjani kabla mechi kuanza.Ni baada ya kupata ripoti hiyo,ndipo FIFA itajua la kusema zaidi.

Serikali ya Ivory Coast nayo iliarifu mwanzoni mwa wiki hii, kwamba inafanya nayo uchunguzi kujua nani wa kubeba dhamana ya vifo hivyo. Mara nyingi visa kama hivyo vimekuwa vikitokea katika viwanja mbali mbali vya dimba barani Afrika:

Licha ya juhudi za FIFA kutaka matengenezo ya viwanja ili kuepusha balaa kama hilo la Abidjan,msiba wa Abidjan ni wapili katika kinyanganyiro cha sasa cha kuania tiketi za finali ya Kombe lijalo la dunia 2010 nchini Afrika kusini.

Hapo Juni, mwaka jana, mashabiki 8 walifariki huko Liberia pale mashabiki walipokanyagana kuingia kwa nguvu uwanajani ambao tayari ulikwisha sheheni mashabiki.Ilikuwa wakati wa mpambano kati ya Liberia na Gambia.

Uchunguzi wa FIFA umegundua hapo August, 2007, kwamba ni viwanja 18 tu vya Afrika vilivyo katika hali ya usalama kuruhusu mashindano ya kuania tiketi za kombe la dunia.Uchunguzi wa FIFA uliingiza viwanja vya nchi 50 za kiafrika.

Tikirejea katika mada ya Kombe lijalo la Dunia, FIFA-shirikisho la kabumbu ulimwenguni,liliarifu kati ya wiki hii kwamba, limershapokea maombi ya tiketi milioni na nusu kwa mashabiki wanaotaka kujionea kombe lijalo la dunia nchini Afrika Kusini.

Mashabiki kutoka nchi 205 wameomba kununua tiketi zao kupitia awamu ya kwanza ya uuzaji tiketi.Wakaazi wa afrika kusini yenyewe wamechukua 30% ya maombi hayo ya viti kiasi cha zaidi milioni na nusu.Watalipa Rand 140 sawa na dola 15 au euro 11.Mashabiki kutoka Marekani ndio waliotia fora kwa maombi wakifuatwa na wale wa Uingereza,Ujerumani,Itali na Australia.Bei kwa mashabiki nje ya Afrika kusini ni dala 80.

Wakati Afrika inajiandaa kwa Kombe lake la kwanza la dunia hapo mwakani 2010, Halmashauri Kuu ya olimpik Ulimwenguni (IOC) iliarifu kati ya wiki hii kwamba Afrika au Amerika kusini yaweza kuandaa michezo ya olimpik ya majira ya

MUANDISHI:Ramadhan Ali

Mhariri:Abdul Mtulya

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com