Kombe la klabu bingwa Afrika uwanjani: | Michezo | DW | 02.04.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Kombe la klabu bingwa Afrika uwanjani:

Bundesliga:Munich yaumana na Wolfsburg:

Grafite(Wolfsbur) hakosi kutia bao,

Grafite(Wolfsbur) hakosi kutia bao,

Baada ya changamoto za kati ya wiki za kinyanganyiro cha kuania tiketi za finali ya Kombe lijalo la dunia mwakani nchini Afrika Kusini ambamo Ujerumani iliitimua nje Wales kwa mabao 2:0,Uingereza ilitamba pia kwa mabao 2:0 dhidi ya Ukraine na mabingwa wa Ulaya-Spain kuwika kwa mabao 2:1 dhidi ya Uturuki, Argentina ikiongozwa na Maradona kuaibishwa na Bolivia kwa mabao 6 :I,Ligi za taifa zinarudi uwanjani mwishoni mwa wiki hii:

Kwa bara la Afrika, kinyanganyiro cha kombe la klabu bingwa-au Champions League kinawakuta mabingwa wa Tanzania Young Africans wakijaribu leo kufuta mabao 3 ya mabingwa Al Ahly ,nyumbani Dar-es-salaam.Kwa Younga asema Ramadhan Ali itakua kama kuparamia mlima kilimanjaro:

Katika duru iliopita mjini Cairo, Young Africans walizabwa mabao 3:0 na ili kusonga mbele ya mabingwa Al Ahly ,wanahitaji mabao 4.Kocha wa Yaounga ameutambua ukweli,lakini viongozi wa younga anasema mwanamichezo wetu George Njongopa huko Dar-waota ndoto:

Mjini Harare, Monomotapa ya Zimbabwe ina miadi na AJAX Cape Town.Mizinga ya Canon Yaounde italengwa langoni mwa waangola: Primeiro Agosto. Kampala City Council imefunga safari hadi Johannesberg kuonana na SuperSport Utd.TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo,timu ya kwanza kulitwaa Kombe hili mara mbili mfulłulizo,wameenda Luanda,kwa miadi yao na Petro Atletico.ZESCO UTD ya zambia inaikaribisha Africa sports ya Ivory Coast wakati mjini Oumduraman, nje ya Khartoum, wanaonana Al-Merreikh na Al-Ittihad ya Libya.Washindi wa duru hii watasonga mbele kwa duru ya mwisho ya kufuzu kugombea Kombe hili.

Huku ulaya, changamoto na FC Barcelona ya Spain katika champiopns League, inapewa leo kisogo na mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich.Macho ya mabingwa yanakodolewa mpambano wa kuamua nani anaparamia kileleni baina ya Munich na Wolfsburg isiokubali kushindwa.Bayern munich inakutana na FC Barcelona jumatano hii ijayo katika zahama za Champions League, lakini leo Munich inataka kuwa timu ya kwanza ya Bundesliga kuthubutu kuwika katika uwanja wa Volkswagebn Arena mjini Wolfsburg.Timu zote mbili-munich na Wolfsburg zina pointi sawa 48 na pointi 1 tu nyuma ya viongozi wa Ligi Hertha Berlin.

Kocha wa zamani wa mabingwa B.Munich, Felix Magath, ame,kinoa kikosi cha wolfsburg barabara na kina makucha makali ambayo yaweza leo kuirarua vipande 2 Munich licha ya kurudi uwanjani kwa m shambgulizi wao Luca Toni,alieumia.Hatima ya Lukas Podolski kuchezeshwa tangu mwanzo leo haijulikani baada ya kurudi Luca Toni,ingawa Miroslav Klose bado si fit.

Mpambano mwengine wa kukata na shoka jioni hii ni kati ya Hamburg na Hoffenheim,viongozi wa Ligi hertha Berlin na Borussia Dortmund.Stuttgart inajiwinda kutamba leo huko Bochum.Kesho jumapili zahama itakua mjini Cologne pale timu 2 za mtaani-FC Cologne na jirani yake Bayer Leverkusen zikikumbana katika derby kuamua nani ni bwana wa dimba kandoni mwa mto Rhein.

Karsruhe inayoburura mkia wa Ligi inajiwinda kesho nyumbani kuzima vishindo vya Borussia Moenchengladbach wakati duru ya mwishoni mwa wiki hii inakamilishwa kesho jioni na Werder Bremen yenye miadi nyumbani na jirani zao Hannover 96.

Ama katika Premier League-ligi ya Uingereza, FC Liverpool,inaazimia kuendelea kuvuma kwa kishindo mwishoni mwa wiki hii na kuitia zaidi kishindo Manchester United-mabingwa.Liverpool wana miadi leo na Fulham.

Baada ya kuzilaza Real Madrid,Manu na hata Aston Villa na kutia mabao 13 katika mechi tatu zilizopita, Liverpool wakati huu iko katika afya njema.hatahivyo, Fulham haityakua mboga kwa Liverpool.Kwani, wao pia wameikomea Manchester United mabao 2-0.Arsenal iliopo nafasi ya 4 ya ngazi ya Ligi,wanacheza na Manchester City wakati Everton wanatamba nyumbani mbele ya Wigan Athletic, hull City inapambana na Portsmoith wakati West Ham inaikaribisha Sunderland.

Muandishi : Ramadhan Ali

Mhariri: Mohammed Abdulrahman