Kombe la Dunia:Ujerumani yacharuka | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 14.06.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Kombe la Dunia:Ujerumani yacharuka

Katika mashidano ya kugombea kombe la dunia nchini Afrika Kusini, Ujerumani imeshinda mechi yake ya kwanza kwa kuichabanga Australia mabao manne kwa bila.

default

Waachezaji wa Ujerumani wakishangalia moja ya mabao manne waliyoifunga Australia

Washambuliaji, Lukas Podolski na Miroslav Klose waliliona lango la Australia katika dakika  30  za kwanza.

Magoli  mawili ya Ujerumani yaliongezwa  katika kipindi cha pili cha mchezo, na Thomas Müller na Cacau.

Hata hivyo katika kipindi cha pili Australia ilibakiwa na wachezaji 10 baada ya Tim Cahill kuonyeshwa  kadi nyekundu kwa  sababu ya kucheza faulo.

Hapo awali Ghana iliibwaga Serbia kwa  bao moja la penalti  baada mchezaji wa Serbia kuunawa mpira ndani ya eneo nyeti katika dakika ya 86.

Kabla ya mechi hiyo Slovenia  ijipatia ushindi wa kwanza katika mshindano ya kombe la dunia kwa kuifunga Algeria bao moja kwa bila.

 • Tarehe 14.06.2010
 • Mwandishi Aboubakary Jumaa Liongo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Nq9W
 • Tarehe 14.06.2010
 • Mwandishi Aboubakary Jumaa Liongo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Nq9W

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com