1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kombe la dunia

3 Desemba 2010

Urusi na Qatar kuandaa kombe la dunia.

https://p.dw.com/p/QOat
Kombe la dunia.

Shirikisho la kandanda duniani FIFA limezifichua nchi ambazo zitaanda mashindano ya kombe la dunia mwaka 2018 na 2022.

Alipokuwa mjini Zürich, Switzerland, mwenyekeiti wa shirikisho hilo Sep Blatter alizitangaza Urusi na Qatar kuwa waandalizi wa mashindano hayo.

Fifa Blatter WM 2018 Russland
Rais wa shirikisho la FIFA Joseph Blatter.Picha: AP

Urusi iliishinda Uingereza pamoja na maombi ya pamoja kutoka kwa Uhispania na Ureno, na Uholanzi na Belgium. Kamati ya FIFA yenye wanachama 22 pia iliichaguwa Qatar kuwa mwandalizi wa mashindano hayo mwaka 2022.

Nchi hiyo ya Ghuba ilizishinda Marekani, Australia,Japan na Korea kusini. Itakuwa ni mara ya kwanza kwa Urusi na Qatar kuandaa mashindano hayo.

Mwandishi:Maryam Abdalla /AFPE.

Mpitiaji:Hamidou Oummilkheir