KOMBE LA DUNIA-GHANA ! | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 26.06.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

KOMBE LA DUNIA-GHANA !

Ghana leo inapambana na Marekani katika raundi ya pili ya kombe la dunia.

default

Washabiki wa timu ya Ghana.

Raundi ya pili ya mashindano ya kombe la dunia inaanza leo nchini Afrika Kusini ambapo timu16 zitashiriki .

Leo Ghana itapambana na Marekani na Uruguay itachuana na Korea ya Kusini.Ghana ndiyo timu pekee ya Afrika iliyobakia katika mashindano ya kombe la dunia.

Ikiwa itafanikiwa kuilaza timu ya Marekani Ghana itakuwa nchi ya tatu ya kiafrika kuingia katika robo fainali baada ya Cameroon na Senegal.Hapo jana bingwa wa Ulaya Uhispania ilifanikiwa kuingia katika raundi ya pili, baada ya kuibwaga Chile kwa mabao mawili kwa moja.

Licha ya kubwagwa, timu ya Chile pia itashiriki katika raundi ya pili.

 • Tarehe 26.06.2010
 • Mwandishi Abdu Said Mtullya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/O3wM
 • Tarehe 26.06.2010
 • Mwandishi Abdu Said Mtullya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/O3wM

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com