1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kombe la dunia 2010

4 Septemba 2008

Ujerumani inarudi uwanjani jumamosi kuania tiketi yake ya kombe la dunia 2010 ikiwa na msukosuko.

https://p.dw.com/p/FBWQ
Ballack na Kanzela MerkelPicha: AP

Mwishoni mwa wiki hii kinyanganyiro cha kuania tiketi za kombe lijalo la dunia 2010 nchini Afrika kusini kitarudi uwanjani takriban katika mabara yote na hasa Afrika,Asia na Ulaya.

Ujerumani ina miadi na chipukizi Liechtenstein hapo jumamosi lakini timu ya Taifa bila nahodha wake Michael Ballack, imekumbwa na msukosuko.

Mfumo wa CAF na FIFA wa kuchanganya tiketi za kombe la Afrika la mataifa na kombe la dunia 2010 huko Angola na Afrika kusini, huenda ukaipiga kumbo Bafana Bafana nje ya kombe la Afrika .

►◄

Tukianza na Ujerumani-inaanza kampeni yake kwa safari ya Afrika kusini 2010 ikiwa bado inaugua pigo ililopata kutoka Spain iliishinda katika finali ya kombe la ulaya 2008.

Kushindwa Ujerumani kwa bao 1:0 na Spian mjini Vienna, Juni 29 kuliongoza kutoleana maneno makali baina ya nahodha Michael Ballack anaeichezea Chelsea na meneja wa timu ya Ujerumani oliver Bierhoff pale ilipolia firimbi ya mwisho uwanjani.Ni walipoingilia kati wachezaji wengine ndipo ugomvi wao ulizimwa.

Mvutano wao ulitokana na kitu gani ndio kwanza inafahamika.Yasemekana kuna mvutano baina ya baadhi ya wachezaji na nahodha wao Michael Ballack ambae wakati huu ameumia.Baadhi ya wachezaji hawaridhiki kucheza jumamosi hii na Liechtenstein bila nahodha Ballack huku mechi yapili ikifuata huko Finland bila yeye. Ballack asemekana amefadhahika mno kwa kushindwa kwa mara nyengine baada ya kombe la dunia kuiongoza Ujerumani kutwaa kombe.

Mvutano wake na Bierhoff umechafua heba ya amani katika timu ya Ujerumani iliojengeka tangu kombe la dunia 2006.

ili kumtuliza shetani,kocha Joachim Loew amezungumza na nahodha Ballack kuhjusu uigomvi wake na Bierhoff pamoja na tabia yake Ballack mbele ya baadhi ya wachezaji.Ballack asemekana amekutana sasa na meneja Bierhoff kumaliza ugomvi.Ni chini ya hali hii,Ujerumani itacheza jumamosi na Liechtenstein.

Taarifa nyengine ya msukosuko katika timu ya Ujerumani ni kuhusu Lukas Podolski na klabu yake ya Bayern Munich.

Podolski ameliambia gazeti la BILD jana kwamba sasa anajuta kwanini alijiunga na Bayern munich kutoka FC Cologne.Angejua kwamba anabidi kupigania nafasi ya kucheza,asingefanya hivyo.

Podolski akichezeshwa kama mchezaji wa akiba wakati wa kocha wa zamani Ottmar Hitzfeld na sasa hali ni hiyo hiyo katika uongozi wa kocha Jurgen klinsmann.

Podolski atazingatia hali yake mwishoni mwa mwaka akifikiria kurudi FC Cologne au kwenda kucheza ngambo.

Hata barani Afrika kumezuka msukosuko unaoweza kuongoza kwa Afrika kusini ,mwenyeji wa kombe lijalo la dunia 2010 isiweze kucheza katika kombe la Afrika la mataifa katika nchi jirani ya Angola mwaka huo.

FIFA-shirikisho la dimba ulimwenguni na CAF-la Afrika wamezusha mtafaruku utakaoilazimu timu ya nchi moja kushindwa au kutoka sare mechi yake ya mwisho ili isonge mbele mashindanoni.Kwani mfumo wa unachanganya kufuzu kwa Kombe la dunia ni pamoja na kufuzu kucheza kombe la Afrika kukiingiza timu zote 2 wenyeji-Angola na Afrika kusini.

Wakati wa kura ya kuzipambanisha timu zinazoania nafasi ya kombe la dunia huko Durban mwaka jana, timu 48 za kanda ya Afrika ziligawanywa makundi 12 ya timu 4-4 pamoja na washindi 12 pamoja na timu 8 bora za nafasi ya pili zikisonga mbele duru ya pili na ya mwisho.

Tatizo likazuka pale Eritrea ilipojitoa kutoka kundi la 11 na hivyo kupelekea kusalia timu 3 tu katika kundi lake.

Ikaamuliwa ili kutafuta timu 8 bora zilizofuata nafasi ya pili,timu zote zilizotokea wapili katika makundi yao ya timu 4 matokeo yao yatafutwa mbele ya timu ya chini kabisa katika orodha.

Katika kundi la 4 ambamo Afrika kusini yakaribia kutolewa nje ya kombe la Afrika,2010,wenyeji hao waweza wakajikuta wanapigwa kumbo endapo wakishinda mechi yao ya mwisho dhidi ya Guinea ya Ekweta....

Na kwavile, hii yaweza kweli kutokea,inastaajabisha kuona FIFA na CAF ziliruhusu mfumo tangu awali unaoilazimisha timu fulani kutoshinda mechi ili iweze kusonga mbele mashindanoni.