Kombe la Afrika laendelea Ivory Coast. | Michezo | DW | 27.02.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Kombe la Afrika laendelea Ivory Coast.

Taifa Stars (Tanzania ) na Chipolopolo (Zambia)

Luca Toni-jogoo la B.Munich

Luca Toni-jogoo la B.Munich

Ushindi wa kishindo kikubwa wa mabao 5-0 wa Bayern Munich katika champions League hapo juzi dhidi ya Sporting Lisbon ya Ureno, umewafunga midomo wakosoaji wa kocha wao Jurgen klinsmann.Kesho lakini Munich inacheza katika pori la simba .Kwani, hata Werder Bremen ilinguruma juzi katika kombe la Ulaya la UEFa ilikoiitimua AC milan ya Itali kwa mabao 2 ya Claudio Pizzaro wa Peru.

Baada ya kuzabwa mabao 2-1 jumamosi iliopita na FC Cologne na kupoteza mechi 3, Munich haidiriki kulazwa tena kesho na bremen ikiwa isizike matumaini yake ya kuvaa taji.

Viongozi wa ligi Hamburg walikuwa pia uwanjani kati ya wiki katika Kombe la UEFA kama Bremen.Mahasimu wao kesho ni Wolfsburg.Hoffenheim iliopo nafasi ya pili ya ngazi ya Ligi nyuma ya Hamburg ina miadi na Borussia Dortmund.Schalke inacheza na Frankfurt.Berlin inatamba nyumbani mbele ya Borussia Moenchengladbach.FC Cologne ilifungua dimba la duru hii jana ilipoikaribisha nyumbani Armenia Bielefeld.

Katika premier League-ligi ya Uingereza ni kufa-kupona kesho kwa Liverpool inayoonana na Middlesbrough. Ikishindwa kufua dafu,Liverpool haitaweza kuizuwia Manchester united kutoroka na mapema na taji la premier League. Chelsea ikiwa pointi 3 nyuma ina miadi na Wifan Athletic baada ya kuanza kutamba ikiongozwa na kocha mpya Guus Hiddink.Arsenal inaikaribisha Fulhal uwanjani mwake Emirates Stadium.

Taarifa zinasema Bundesliga, ligi ya Ujerumani, ndio inayotia fedha nyingi kabisa kuliko Ligi yoyote barani Ulaya kwa kutembeza jazi za timu zake kwa wafadhili-sponsors. Hii ni kwa muujibu wa ripoti ya jazi ya Ulaya mwaka 2008/09 iliotoka wiki hii.Timu 18 za Bundesliga zimevuna kitita cha euro milioni 102.9 sawa na dala milioni 130.5 kwa msimu huu kutokana na kutembeza jazi zao kwa wafadhili na hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa Bundesliga kuvuka kima cha euro milioni mia 1.Haisangazi kwahivyo kuona mabingwa wa ujerumani Bayern Munich iko kileleni ikiwa imevuna Euro milioni 20 kwa kutembeza jazi zake.

Jumla ya fedha za kutembeza jazi katika nchi 6 zinazoongoza kwa ligi zao baraniUlaya:Uingereza,Spian,Itali,Ujerumani , Ufaransa na Holland zimepungua kwa kima cha Euro milioni 393.2 -sababu kuu taarifa zinasema ni kuteremka thamani ya pauni ya Uingereza kulikofanya thamani ya fedha zilizopatikana kutoka kutembeza jazi zao kwa wafadhili ikiteremka hadi Euro 85.9 milioni. Na licha ya msukosuko wa mabanemki, mabenki ndio bado yanayochangia mno hadi euro milioni 80.7 katika kufadhili klabu-hiki ni kima cha euro milioni 30 zaidi kuliko sekta nyengine.

Huko Ivory Coast jumamosi jioni ni kinyanganyiro cha Kombe la Afrika la mataifa kwa wachezaji wa ndani ya Afrika kinaendelea: Taifa Stars-Tanzania, ina miadi na jirani zao "Chipolopolo" -Zambia .Iwapo Taifa Stars itaweza kukwepa isipopolewe nje na risasi za Chipolopolo, ni firimbi ya mwisho itatwambia.Kuwsili hatua hii,Tanzania ilwatoa wenyeji Ivory Coast kwa bao 1:0 juzi jumatano.nusu-finali zitakuwa jumatano ijayo.