Kombe la Afrika la klabu bingwa | Michezo | DW | 06.08.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Michezo

Kombe la Afrika la klabu bingwa

Etoile du sahel ya tunisia ni ya kwanza kui ngia nusu-finali ya kombe la klabu bingwa.Muethiopia Gebreselassie atamba katika New York-marathon.

Natuanze lakini na duru ya kwanza ya changamoto za kombe la shirikisho la dimba la Ujerumani lililofungua pazia mwishoni mwa wsiki la msimu mpya wa Bundesliga-ijumaa hii.

Maajabu 2 yalitokea;Schalke 04-makamo-bingwa wa ujerumani walianza msimu kwa kishindo walipoizaba Eintracht Trier ya daraja ya 5 mabao 9:0.Mjerumani wa asili ya Ghana,Gerald Asamoah alitia pekee mabao 3-hattrick.

Msangao mwemngine uliozuka jana ni FC Cologne, inayotapia kurudi daraja ya kwanza msimu ujao, ilitolewa katika kombe hilo la shirikisho na timu ya wachezaji wa akiba ya werder Bremen ilipochapwa mabao 4-2 baada ya kurefushwa mchezo.Bremen inacheza daraja ya tatu.

Hata timu jirani na Cologne, Bayer Leverkusen ilikiona kilichomtoa kanga manyoya.Ilichapwa bao 1:0 na St.pauli ya daraja ya pili-maadui wa FC Cologne,katika duru ya kwanza ijayo ya Bundesliga.

Mabingwa watetezi wa kombe hili Nüremberg,waliitandika timu ya daraja ya 5 Viktoria Hamburg mabao 6:0.Leo itakua zamu ya Bayern munich kucheza na klabu ya daraja ya 3 ya Wacker Burghausen.Je, itatiwa nayo munda ?

Mabingwa wa Uingereza Manchester united wamewatandika mabingwa wa kombe la FA –kombe la chama cha mpira cha uingereza mabao 3-0 kupitia mikwaju ya penalty.Hapo kabla zilisimama sare bao 1:1 mwishoni mwa dakika ya 90 ya mchezo.

Tugeukie sasa kinyan’ganyiro cha kombe la klabu bingwa barani afrika na kombe la shirikisho-Confederations cup:

Katika kombe la shirikisho,kocha wa wa Kwara United nusuzra akione kilichomtoa kanga manyoya:

Mashabiki wa Kwara wakiwa hawakuridhika na sare ya bao 1:1 na Ismailia ya Misri tena nyumbani Ilorin, walitaka kulipiza kisasi chao kwa kocha wao.Polisi walibidi kumuokoa.

Katika kombe la klabu bingwa, Etoile du sahel ya Tunisia, imekuwa timu ya kwanza kukata tiketi yake ya nusu-finali.

Etoile ni klabu iliotamba sana katika dimba la Afrika.Klabu hii ya Sousse, imelitwaa kombe la shirikisho,kombe la super cup la afrika, kombe la washindi na kombe la CAF tangu kuibuka kilelelni mwa dimba la afrika miaka 12 iliopita.

Mabingwa Al Ahly, wamevunjiwa rekodi yao ya kutoshindwa mfululizo wa mapambano 7 walipozabwa bao 1:0 na esperence-klabu nyengine ya Tunisia.

ASEC Abidjan ya Ivory Coast,ilitamba jana kwa bao 1:0 mbele ya Al hilal ya Sudan.

Katika medani ya riadha, bingwa wa mabingwa Haile Gebreselassie,alitamba jana katika mbio za nusu-marathon za New York.Muda wake wa ushindi ulikuwa dakika 59 na sek.24.

Gebre alifyatuka mbio na kuwaacha wenzake 3 katika hatua ya maili 8 karibu na Times Square na kuanzia hapo hakuna alieweza kumkamata.Muda wake ni wapili kurekodiwa katika mbio za nusu-marathon nchini Marekani.

Bingwa wa sasa wa Boston na Chicago marathon Robert Cheruiyot kutoka Kenya,alibidi mara hii kuridhika na nafasi ya 3.Baadae Cheruiyot alipelekwa hospitali kukaguliwa hali yake.

Ama upande wa wasichana Hilda Kibet wa Kenya alimpita kwa sek. 1 tu mwenzake Catherine Ndereba kushinda.Muda wake ulikuwa 1:10:32.

Mwishoe,tumalizie michezo ya olimpik 2008 mjini Beijing:Maandalio ya michezo hiyo ambamo wanariadha wa Afrika wanajiandaa kutamba yanakwenda sawa sawa-waandazi wamearifu leo.Viwanja vyote vya michezo vitakuwa tayari mwishoni mwa mwaka huu na uuzaji wa tiketi za kiingilio pia unaenda uzuri.

 • Tarehe 06.08.2007
 • Mwandishi Ramadhan ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHbT
 • Tarehe 06.08.2007
 • Mwandishi Ramadhan ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHbT