1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kocha wa Spain asifu uwezo wa kikosi chake Euro 2024

10 Julai 2024

Kocha wa Uhispania ameusifu ubora wa kikosi chake ambacho kilifanikiwa kupindua mezani na kuishanda Ufaransa katika mchezo wa nusu fainali wa michuano ya EURO 2024 uliopigwa usiku wa kuamkia leo mjini Munich.

https://p.dw.com/p/4i6IA
Euro 2024 | Ujerumani | Luis de la Fuente
Kocha wa kikosi cha Uhispania Luis de la Fuente Picha: Thilo Schmuelgen/REUTERS

De la Fuente amesema wachezaji wake wameonesha uwezo mkubwa wa kubadili mchezo haraka na kwa pamoja walimudu kuizidi Ufaransa maarifa na kujikatia tiketi ya kucheza fainali ya siku ya Jumapili.

Soma pia:Uhispania yaishinda Ufaransa 2-1 kufika fainali ya EURO 2024

Kwenye huo uliotimua vumbi katika dimba la Allianz Arena, Uhispania ilipata ushindi wa bao 2-1 hata baada ya Ufaransa kutangulia kupata goli la kwanza la mnamo dakika za mapema. 

Uhispania sasa inasubiri matokeo ya mchezo wa nusu fainali ya leo unaozikutanisha England na Uholanzi ili kufahamu timu watakayokutana nayo fainali za Julai 14 mjini Berlin.