1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kocha wa Barca akanusha ripoti za mvutano kikosini

Bruce Amani
29 Juni 2020

Nchini Uhispania mbio ya ubingwa wa ligi kuu La Liga zimeshika kasi kati ya vinara Real Madrid na mabingwa watetezi Barcelona. Kuna ripoti za mvutano kikosini madai ambayo yamekanushwa

https://p.dw.com/p/3eWMK
Fussball l Neuer Trainer bei FC Barcelona - Quique Setien
Picha: Reuters/A. Gea

Kocha wa Barca Quique Setien amesisitiza kuwa uhusiano wake na wachezaji ni mzuri, licha ya ripoti kuwa kuwepo ugomvi kikosini na mvutano kati ya Lionel Messi na naibu wa Setien, Eder Sarabia. "Uhusiano tulio na wachezaji ni mzuri. Ni kweli kwamba wakati mwingine ambapo mtu hukubaliana au kutokubaliana na kitu, lakini sioni tatizo lolote ambalo ni la kuzungumzia." Amesema Setien

Kulizuka majibizano baada ya sare ya 2 – 2 ya Barcelona na Celta Vigo matokeo yaliyowaweka Real Madrid kuchukua usukani na pengo la pointi mbili kwa kuwafunga Espanyol 2 – 0.

Msukosuko huo unakuja wakati mbaya ikizingatiwa kuwa Barca wanawaalika Atletico Madrid kesho Jumanne na hawahitaji kuteleza tena.