Klabu ya Zamalek kuadhibiwa baada ya kutofika uwanjani
26 Februari 2020Matangazo
Shirikisho la kandanda nchini Misri EFA limeomba radhi kwa mashabiki baada ya mchezo huo kufutwa na kusema katika taarifa leo kuwa sheria zake za kinidhamu zitatumika. Zamalek haikuwasili uwanjani kwa ajili ya mchezo huo ikipinga dhidi ya vikwazo vikali vilivyotolewa dhidi ya wachezaji wake na maafisa kutoka vilabu hivyo viwili baada ya kupigana wakati timu hizo zilipokutana mjini Abu Dhabi wiki iliyopita katika mpambano wa kombe la Super Cup.
Rais wa Zamalek Mortada Mansour ni miongoni mwa wale walipigwa faini na amepigwa marufuku baada ya mchezo huo, ambao walishinda kwa mabao 4-3 kupitia mikwaju ya penalti baada ya kutoka sare bila kufungana.