1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiungo Aranguiz kutoichezea Leverkusen kwa miezi kadhaa

21 Agosti 2015

Kiungo wa Chile Charles Aranguiz atakuwa mkekani kwa muda mrefu baada ya kuumia mishipa ya kisigino, wiki moja tu baada ya kujiunga na Bayer Leverkusen. Mkurugenzi wa spoti wa klabu hiyo amesema ni pigo kubwa

https://p.dw.com/p/1GJSY
Charles Aranguiz Leverkusen Fußball Bundesliga 2015
Picha: picture-alliance/dpa/F.Gambarini

Klabu hiyo ya Bundesliga imesema Aranguiz aliumia wakati akiwa mazoezini siku ya Alhamisi jioni na atarajiwa kufanyiwa upasuaji mjini Basel, Uswisi Jumanne wiki ijayo.

Atakuwa nje kwa miezi kadhaa na huenda asicheze tena mwaka huu. Mkurugenzi wa spoti wa Leverkusen Rudi Voeller amesema wahuzunishwa na habari hizo na pigo kubwa kwao. Ameongeza kuwa watafanya kila wawezalo kuhakikisha kuwa mchezaji huyo anapona haraka iwezekanavyo na kurejea uwanjani.

Aranguiz ni koungo mkabaji ambaye aliripotiwa kuigharibu Leverkusen euro milioni 12 na alisajiliwa kuipiga jeki klabu hiyo ya Ujerumani katika safu ya kiungo baada ya kuongoka kwa wachezaji wa timu ya taifa ya Ujerumani Gonzalo Castro na Stefan Reinartz na pia kustaafu kwa Simon Rolfes.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Iddi Sessanga