1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kisa cha mwanasiasa wa CDU aliyeangushwa kwa sababu ya mapenzi

15 Agosti 2011

Mwanasiasa wa chama cha CDU katika jimbo la Schleswig-Holstein ateleza kwakufanya mapenzi na msichana wa miaka 16 na hali nchini Somalia imemulikwa magazetini Abuu

https://p.dw.com/p/12Ghf
Christian von BoetticherPicha: picture-alliance/dpa

Tuanzie lakini na gazeti la "Westfällische Nachrichten la mjini Münster linaloandika:

Hata kama kimandhari jimbo hilo linalozungukwa na bahari ni la kuvutia, kisiasa lakini mawingu ya kashfa yametanda. Ikiwa mwaka 2005 uchaguzi wa siri uliwawezesha wanasiasa fulani kumtoa madarakani aliyekuwa wakati ule waziri mkuu wa Schleswig Hostein, hivi sasa mgombea nyota wa chama cha CDU Christian von Boetticher ameteleza kwa sababu ya kufanya mapenzi na msichana mwenye umri wa miaka 16. Miezi tisa kabla ya uchaguzi katika jimbo hilo, CDU inajikuta katika kizungumkuti, wakitanguliwa na waziri mkuu anaemaliza wadhifa wake Peter Harry Carstensen lakini bila ya kuwa na mwanasiasa anaewekewa matumaini.

Gazeti la Flensburger Tageblatt linasema:

Christian von Boetticher ameporomoka lakini sio kwasababu ya mapenzi, bali kwa uzembe wake mwenyewe. Ni balaa kubwa hilo kwake na msiba kwa chama cha CDU katika jimbo la Schleswig Holstein. Miezi tisa kabla ya uchaguzi jimboni humo, wana CDU wanajikuta katika hali ya kutatanisha inayohitaji kubadilishwa. Kimsingi kadhia hiyo inafungua fursa njema. Tangu miezi kadhaa sasa hali imekuwa ikitokota tangu chamani mpaka miongoni mwa kundi la wabunge wa chama hicho kwa sababu watu walikuwa wakihisi shughuli za kisiasa za Boetticher haziridhishi. Kwa hivyo pengine kwa wengine miongoni mwa wana CDU wa jimbo hilo la kaskazini, kadhia hii imejiri wakati ndio hasa. Njia sasa iko wazi kuuchagua uongozi mpya."

Christian von Boetticher CDU NO FLASH
Christian von BoetticherPicha: picture-alliance/dpa

Gazeti la "Nordwest-Zeitung" linajiuliza

Kama CDU itafanikiwa kumpata mgombea mwengine mwenye nafasi nzuri ya kuchaguliwa na walio wengi hadi uchaguzi utakapoitishwa mwezi Mei mwakani katika jimbo hilo. Kuna wanaoshuku. Hilo ni pigo kubwa pia kwa chama cha FDP ambacho kinyume na hali namna ilivyo katika daraja ya shirikisho, kimekuwa kikitarajia kurefusha serikali ya muungano pamoja na chama cha CDU katika jimbo hilo. Kama SPD watafaidika na hali hiyo, hakuna pia ajuae. Meya wa jiji la Kiel Torsten Albig aliyependekezwa na waziri wa zamani wa fedha Peer Steinbrück atapigania wadhifa huo, hata hivyo umashuhuri wake una kikomo.

Na ripoti yetu ya mwisho magazetini inahusiana na hali nchini Somalia. Gazeti la "Dresdner Neueste Nachrichten" linaandika:

Hungersnot in Somalia
Wakimbizi wa SomaliaPicha: dapd

Tatizo kubwa bado linahusu namna ya kuweza kuwafikishia misaada watu wanaosumbuliwa na njaa katika nchi hiyo inayozongwa na vurugu na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Rushwa, wanamgambo wanaoranda randa na ukosefu wa sheria yote haya si mapya barani Afrika. Hawajakosea wanaosema maafa yangeweza kuepukwa kwa sababu tangu mwanzo yalikuwa yakijulikana.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir

Mhariri:Josephat Charo