Kipchoge: Sikio langu la kulia liliziba | Michezo | DW | 05.10.2020
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Kipchoge: Sikio langu la kulia liliziba

Mfalme wa mbio za masafa marefu marathon Eliud Kipchoge kutoka Kenya anasema alishindwa kulitetea taji lake la mbio za London Marathon jana kwa kuwa alipata changamoto mbio zilipokuwa katikati.

"Mbio zilikuwa nzuri nilianza vyema, kulikuwa na baridi lakini nilipata tatizo dogo tu na sikio langu la kulia, liliziba na nilijaribu kulizibua ila haikuwezekana. Ila yote tisa huu ni mchezo na katika michezo leo utakuwa juu kesho utakuwa chini," alisema Kipchoge.

Hii ilikuwa ni marathon ya pili Kipchoge kushindwa katika taaluma yake hiyo ya ukimbiaji wa mbio za masafa marefu.