Kiongozi wa zamani wa Indonesia Suharto amefariki hospitali | Habari za Ulimwengu | DW | 27.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Kiongozi wa zamani wa Indonesia Suharto amefariki hospitali

JAKARTA:

Kiongozi wa zamani wa Indonesia,Suharto amefariki dunia akiwa na miaka

86.Kiongozi huyo alikuwa akiugua tangu muda mrefu na alipelekwa tena hospitali katika mji mkuu Jakarta wiki tatu za zilizopita.Suharto alitawala nchini Indonesia kuanzia mwaka 1967 hadi 1998.Hadi wanasiasa elfu moja wa upande wa upinzani waliuawa wakati wa utawala wake mrefu wa mabavu.

Aliondoka madarakani kufuatia maandamano makubwa ya upinzani kuhusika na ulajirushwa na ukiukaji wa haki za binadamu.Licha ya kukabiliwa na mashtaka ya ubadhilifu wa mali ya serikali na ukiukaji wa haki za binadamu,mawakili wake walifaulu kumzuia kufikishwa mahakamani kwa sababu ya hali mbaya ya afya.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com