Kiongozi wa Georgia ashinda uchaguzi na wapinzani wakataa | Habari za Ulimwengu | DW | 07.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Kiongozi wa Georgia ashinda uchaguzi na wapinzani wakataa

TIBLIS:

Matokeo ya mwanzo kutoka uchaguzi wa urais nchini Georgia yanaonyesha kama rais Mikhael Saakashvili amepata zaidi ya kura asilimia 50 ya kura zote ambazo zimepigwa.

Matokeo haya yatampauwezo kuepuka marudio ya uchaguzi dhidi ya mpinzani wake wa karibu katika kipindi cha wiki mbili kutoka sasa.Maelefu ya wafuasi wa upande wa upinzani wameandamana katika mji mkuu wakidai kuwa kumefanyika mizengwe kumpendelea.

Hata hivyo wachunguzi kutoka shirika la usalama na ushirikiano la Ulaya wamesema wametosheka na uchaguzi.

Mkuu wa rume ya uchaguzi ya Georgia ameiambia Duesche Welle kuwa huenda wiki mzima ikapita kabla ya kujua matokeo yote.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com