1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kinyang'anyiro kuwania nafasi muhimu Bundesliga chaendelea

Deo Kaji Makomba
25 Juni 2020

Klabu ya Bayern Munich itamaliza msimu wa ligi kuu ya soka Bundesliga ikiwa katika nafasi ya kwanza, na klabu ya Paderbon ikimaliza msimu wa ligi hiyo ikiwa katika nafasi ya 18.

https://p.dw.com/p/3eKnu
Fußball Bundesliga 33. Spieltag | Hertha BSC vs. Bayer 04 Leverkusen
Picha: Getty Images/AFP/M. Sohn

Zimesalia mechi tatu muhimu zitakazoamua nafasi za timu, mechi hizo zikitarajiwa kuchezwa Jumamosi tarehe(27.06.2020) ikiwa ni mechi za mzunguko wa 34 na za mwisho katika msimu huu wa ligi kuu ya soka ya Ujerumani Bundesliga.

Borussia Moenchengladbach na Bayer Leverkusen zimeimarisha katika nafasi ya nne na ya tano, huku timu zinazomaliza msimu katika nafasi za juu zikijishindia mamilioni ya yuro kutoka ligi ya mabingwa Ulaya.

RB Leipzing, ikishikilia nafasi ya tatu bado haijajihakikishia kuilinda nafasi hiyo kutokana na ushindani ulivyo, lakini tofauti ya mabao matatu na faida ya point tatu hakika itawafanya kumaliza ligi wakiwa katika tano bora.

Vilabu vya Wolfsburg na Hoffenheim vyote kwa pamoja vimekwishajihakikishia nafasi ya kucheza ligi ya soka barani Ulaya zikiwa katika nafasi ya sita na saba katika msimamo wa ligi kuu ya soka ya Bundesliga inayoelekea ukingoni hivi sasa.

Vilabu hivyo vinatofautiana tu katika tofauti ya magoli lakini nafasi ya juu ina mapumziko ya muda mrefu katika kipindi cha majira ya joto na timu zilizoko chini zinatakiwa kupambana ili kuweza kufaulu.

Bayern München wameshatawazwa washindi wa msimu huu
Bayern München wameshatawazwa washindi wa msimu huuPicha: Imago Images/Sven Simon/F. Hoermann

Klabu ya Paderbon tayari imekwishashuka daraja lakini Werder Bremen na Fortuna Dusseldorf bado zinakabiliwa na uwezekano wa kuifuata huko, au bahati ya kunusurika na kiusalia katika daraja la kwanza.

Mvutano wa kuwania nafasi ya kucheza ligi ya mabingwa.

Borussia Moenchenladbach iliyoko katika nafasi ya nne ikiwa na alama 62 na tofauti ya magoli 25 itafuzu kucheza ligi ya mabingwa endapo kama watashinda nyumbani dhidi ya Hertha Berlin.

Bayern Leverkusen yenye alama 60 na tofauti ya magoli 16 itafaulu kucheza ligi ya mabingwa barani Ulaya kama itashinda mchezo wake dhidi ya Mainz na Gladbach ipoteze mechi yake dhidi ya Herth.