Kinyang′anyiro cha wademokrats chazidi kuwa kitendawili | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 23.04.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Kinyang'anyiro cha wademokrats chazidi kuwa kitendawili

-

PHILADELPHIA

Hillary Clinton ameshinda uchaguzi wa awali wa jimbo la Pennsylvania dhidi ya mpinzani wake Barack Obama.Hillary Clinton amepata asilimia 53 ya kura dhidi ya asilimia 47 za Barack Obama.Akizungumza punde baada ya kutangazwa mshindi aliwashukuru wakaazi wa Pennsylvania kwa kuwa na imani nae juu ya masuala mbali mbali ikiwemo vita vya Iraq na Afghanstan.Ushindi huo wa Clinton unamfanya kupumua kiasi kutokana na shinikizo zilizokuwa zikitolewa na baadhi ya wademokrats za kumtaka ajitoe kwenye kinyang'anyiro cha kuwania uteuzi wa mgombea wa chama hicho katika uchaguzi mkuu na kumuachia seneta Barack Obama.

Kutokana na matokeo hayo ya uchaguzi wa awali wa jimbo la Pennsylvania Clinton amejiongezea idadi jumla ya wajumbe na kufikisha wajumbe 1,537 ingawa Barack Obama bado anaaongoza kwa idadi hiyo jumla ya wajumbe ambapo anaungwa mkono na wajumbe 1,648. Ili kuteuliwa kuwa mgombea wa chama cha Demokratic katika uchaguzi wa urais unahitajika kuungwa mkono na idadi jumla ya wajumbe 2,025.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com