Kinyang′anyiro cha wademocrats chaendelea Mississippi | Matukio ya Kisiasa | DW | 11.03.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Kinyang'anyiro cha wademocrats chaendelea Mississippi

Obama anapewa nafasi nzuri ya kushinda katika mji wa kusini wa Mississippi hii leo

default

Barack Obama na mpinzani wake chamani Hillary Clinton


Mgombea mwenza wa chama cha Democratic cha Marekani, Barack Obama amesema dhamiri yake ni kua rais wa Marekani na sio makamo wa rais kama alivyoshauri senetor wa New York Hillary Clinton.Matamshi hayo ameyatoa katika wakati ambapo senetor huyo wa Illinois anapewa nafasi nzuri ya kushinda mashindano ya kuania tikiti ya chama cha Democrat kwa uchaguzi wa rais,mashindano yanayofanyika hii leo huko Mississippi."Nimeshinda kura nyingi zaidi ya senetor Clinton,nna idadi kubwa zaidi ya wajumbe,kwa hivyo sielewi vipi mtu ambae anashikilia nafasi ya pili anaweza kupendekeza makamo wa rais awe mtu mwenye kushikilia nafasi ya kwanza-amejiuliza kwa mshangao Barack Obama mbele ya umati wa mashabiki wake.


Senetor huyo kijana amechambua mambo mawili anayosema yanatatanisha:Anasema tunanukuu:wiki mbili  au tatu hivi zilizopita, Clinton na watu wake walisema hawaamini kama nnaweza,kama niko tayari.Sielewi,kama siko tayari, sasa imekwenda kwendaje wakafika hadi ya kushauri niwe makamo wa rais?Amejiuliza na kusababisha kicheko kikubwa miongoni mwa wafuasi wake.


Uwezekano wa kushirikiana na Obama umezushwa na Hillary Clinton wiki iliyopita,aliposhinda katika miji mitatu na kwa namna hiyo kujibwaga upya katika kinyang'anyiro cha kuania tikiti ya chama cha Democratic kwa uchaguzi wa rais wa November ijayo.


"Mkiwaleta pamoja, hakuna atakaeweza kuwazuwia-aliashiria hapo awali mumewe,rais wa zamani wa Marekani,Bill Clinton.


Kinyang'anyiro cha kuania tikiti ya chama cha Democratic kinaendelea hii leo  katika mji wa kusini wa Mississipi ambako Barak Obama anapewa nafasi nzuri ya kushinda. Duru nyengine muhimu itakua Pennsylvania, April 22 ijayo.


Barak Obama  hadi sasa amejipatia uungaji mkomno wa wajumbe wengi zaidi kuliko Hillary Clinton ,hata hivyo hakuna hata mmoja kati yao anaetazamiwa kujipatia wajumbe 2025 wanaohitajika kuweza kuteuliwa.Uamuzi wa mwisho unasubiriwa mkutano mkuu wa wa-Democrats utakapoitishwa Agosti ijayo huko Denver.


Kambi ya Obama iliyoshuhudia kuteleza baadhi ya washauri wake wa siasa ya nje,imewauliza maoni yao viongozi kadhaa wa zamani wa Pentagon tangu wa enzi ya Jimmy Carter mpaka kufikia utawala wa Bill Clinton ambao wote wamekiri ,senetor wa Illinois ana sifa zote zinazostahiki kuweza kua mkuu wa vikosi vya wanajeshi wa Marekani.


Wadadisi hata hivyo wanajiuliza kama kisa kinachomhusisha mshirika wake mkubwa,gavana wa New York Eliot Spitzer  na mambo ya danguro ,kitamharibia kampeni yake ya uchaguzi au la.Mwanasiasa huyo ameomba  radhi baada ya gazeti la New-York Times kufichua kisa hicho na habari za hivi punde zinasema Eliot Spitzer hatojiuzulu wadhifa wake.►◄

 • Tarehe 11.03.2008
 • Mwandishi Hamidou, Oumilkher
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/DMhw
 • Tarehe 11.03.2008
 • Mwandishi Hamidou, Oumilkher
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/DMhw
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com