Kinyang′anyiro cha Ligi ya Premier chapamba moto | Michezo | DW | 03.04.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Kinyang'anyiro cha Ligi ya Premier chapamba moto

Tottenham Hotspur watatumai kupewa msaada kutoka kwa mmoja wa mahasimu wao wanaowania nafasi ya nne bora wakati wakilenga kukifufua tena kinyang'anyiro cha ubingwa wa ligi ya Premier

Wakiwa pointi saba nyuma ya vinara Chelsea, nambari mbili Spurs na pengo la pointi saba kati yao, wanasafiri kucheza dhidi ya Swansea wanaopambana kuepuka kushushwa daraja wakati Chelsea wataantgushana na Manchester City wakilenga kuepuka kichapo cha pili mfululizo.

Wiki moja iliyopita, kinyang'anyiro cha ubongwa kilionekana kuwa kimekishwa kabisa lakini sasa kitarejea tena kama Chelsea, waliozabwa na Crystal Palace nyumbani mwishoni mwa wiki, watazabwa tena nyumbani dhidi ya Manchester City Jumatano wiki hii.

Nambari tatu Liverpool huenda watakosa huduma za Sadio Mane ambaye ni majeruhi, wakati watakutana na Bournemouth. Liverpool waliwazaba Everton 3-1 na wana pointi moja juu ya Man City ambapo walitoka sare ya 2-2 na Arsenal ijapokuwa wamecheza mechi moja zaidi.

Manchester United ambao walitoka sare ya 0-0 nma West brom watasuka dimbani dhidi ya Everton kesho Jumanne, na kama mambo yalivyo, itakuwa vigumu kumaliza katika nne bora. Arsenal watakwaruzana na West Ham United.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/Reuters
Mhariri: Iddi Ssessanga

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com