1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA:Watu 100 washukiwa kuwa na virusi vya Ebola

14 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBPo

Watalaam wa afya katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo wanawasaka takriban watu 100 wanaoaminiwa kuwa walikaribiana na watu walioambukizwa virusi vinavyo sababisha ugonjwa wa Ebola.

Katibu mkuu katika wizara ya afya bwana Benoit Kebelo amesema serikali ya Kongo inawasaka watu hao katika maeneo ya Kampungu kilomita 300 kutoka makao makuu ya jimbo la Kananga.

Wakati huo huo wanajeshi wa kulinda amani katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo wamegundua makaburi matatu ya jumuiya katika eneo la mashariki mwa Kongo.

Makaburi hayo yamepatika katika eneo la Rubare kilomita 60 kaskazini mwa mji wa Goma mji mkuu wa jimbo la Kivu ya kasakzini,eneo ambalo lilikabiliwa na vita kati ya majeshi ya serikali na kikosi kinacho mtii jenerali muasi Laurent Nkunda.

Miili kadhaa imepatikana ndani ya makaburi hayo na wachunguzi wa umoja wa mataifa wanachunguza matukio hayo.

Haijajulikana bado miili hiyo ni ya kina nani, walikufa vipi na ni miili mingapi iliyozikwa ndani ya makaburi hayo.

Eneo la Rubare ni eneo lililokuwa chini ya kanali Innocent Nzalunida wa kikosi kinachomtii jenerali Laurent Nkunda.