KINSHASA:Takriban 30 wauawa baada ya ndege ya mizigo kudondoka | Habari za Ulimwengu | DW | 04.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KINSHASA:Takriban 30 wauawa baada ya ndege ya mizigo kudondoka

Ndege ya moja ya mizigo imedondoka katika eneo la makazi ya watu yaliyo karibu na uwanja mkuu wa ndege mjini Kinshasa na kusababisha vifo vya takriban watu 30.Nyumba kadhaa zinaripotiwa kushika moto katika eneo hilo la Kisangani baada ya ndege hiyo kudondoka.Kulingana na kamanda wa polisi wa eneo hilo Alexis Dekikobo maiti zimeonekana kwenye kifusi cha ndege hiyo. Kwa mujibu wa mkuu wa safari za ndege Alphonse Ilunga miili 19 imetolewa kwenye vifusi hivyo.Kulingana na ripoti ya abiria waliokuwemo kwenye ndege hiyo watu 16 walikuwamo safarini ila wengine wanafahamika kupanda ndege hiyo kabla kuondoka.Chanzo cha ajali hiyo bado hakijulikani na idadi kamili ya abiria.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com