1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA:mvutano umeshtadi saa chache kabla ya uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo

29 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCyF

Saa chache kabla ya kufanyika raundi ya pili ya uchaguzi wa rais nchini JK Kongo, mvutano umeshtadi nchini humo.

Katika kinyang’aricho hicho rais wa sasa bwana Joseph Kabila anapambana na mpinzani wake mkuu bwana Jean Pierre Bemba aliekuwa kiongozi wa waasi katika miaka ya nyuma. Katika raundi ya kwanza ya uchaguzi huo ilioyofanyika mnamo mwezi julai bwana Kabila hakufanikiwa kupata zaidi ya asilimia 50 ya kura ili kuweza kushinda na kuunda serikali peke yake.

Rais huyo wa sasa amesema kwamba hali sasa ni ya mvutano nchini na kwamba hatua zote zinazolazimu zimechukuliwa kabla ya uchaguzi kufanyika baadae leo.

Rais Kabila na mpinzani wake bwana Bemba pia wametoa mwito wa pamoja kwa watu wanaowaunga mkono kuwataka wawe watulivu. Katika tamko hilo mahasimu hao wamejiwajibisha kuhakikisha usalama wakati wa uchaguzi.