1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA:Laurent Nkunda avunja makubaliano ya kusimamisha vita

9 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7HQ

Kiongozi wa kundi la waasi katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo jenerali Laurent Nkunda amesema kwamba amekiuka makubaliano ya kusimamisha mapigano katika eneo la mashariki ya Kongo yaliyofikiwa kati yake na serikali.

Nkunda amevilaumu vikosi vya serikali kwa kushambulia vijiji vya magharibi mwa mji mkuu wa jimbo la Goma.

Jeshi la Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo limethibitisha kuzuka tena kwa mapigano katika eneo la mashariki.