1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA:Kambi ya Bemba yadai kuna njama za udanganyifu

9 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCum

Kambi ya mgombea wa Urais Jean Pierre Bemba imedai kwamba kumekuwepo na udanganyifu katika matokeo ya mwanzo ya ya uchaguzi yaliyochapishwa hivi karibuni.

Msemaji wa makamu wa rais Jean Pierre Bemba,Eve Bazaiba amesema Matokeo hayo ambayo hayajakamilika yaliyochapishwa Novemba 5 ni kinyume na ukweli wa mambo.

Tume ya uchaguzi nchini Kongo hata hivyo ilitangaza kwamba matokeo hayo sio kamili na yanaweza kubadilika wakati wowote.

Kwa mujibu wa Taarifa za shirika la habari la AFP hadi sasa matokeo hayo yanaonyesha ushindi wa rais kabila kwa asilimia 65.69 baada ya kura kuhesabiwa katika wilaya 73 kati ya 169 huku Bemba akiwa na asilimia 34.31 pekee.