1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA:juhudi za uokozi zaendelea baada ya treni kudondoka

3 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBcS

Ujumbe wa Umoja wa mataifa nchini Kongo unatoa huduma za afya baada ya ajali ya treni kutokea hapo jana.Yapata watu 100 wamepoteza maisha yao katika ajali hiyo na wengine 120 kujeruhiwa vibaya.Wengine wengi wanaripotiwa kunasa kwenye mabehewa ya treni hilo lililodondoka.

Madaktari,manesi,watoaji wa huduma za dharura aidha vifaa vya uokozi vyote vimefikishwa kwenye eneo la mkasa..Ujumbe wa Umoja wa Mataifa ulipeleka helikopta moja hii leo kutoka eneo la Kananga iliyowasafirisha madaktari na manesi ili kuwahudumia majeruhi wa ajali jiyo.

Kulingana na abiria walionusurika treni hiyo ilikuwa katika mwendo wa kasi sana wakati mabehewa yake manane yalipodondoka karibu na eneo la Kakenge magharibi mwa jimbo la Kasai.Treni hiyo ilikuw ainaelekea mji wa Kananga.Idadi kamili ya abiria waliokuwamo safarini bado haijulikani.