1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA:Hali mashariki ya Kongo ni ya kutatanisha

21 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBpo

Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa linatiwa wasiwasi na ongezeko la ghasia katika eneo la mashariki ya Kongo.Kwa mujibu wa Balozi wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa Jean-Marc de la Sabliere aliyekuwa ziarani na wajumbe wengine 15 hali ya usalama ni ya kutatanisha.Wajumbe hao walizuru mashariki ya Kongo wakiwa katika ziara yao ya bara la Afrika.

Eneo la Mashariki ya Kongo linalopakana na nchi ya Rwanda linashambuliwa na waasi wa zamani wa Rwanda wanaoaminika kuwa na kambi zao nchini Kongo baada ya kufurushwa nchini mwao.Waasi wa KiHutu wanaaminika kusababisha vifo vya watu 24 mwezi jana.Baadhi yao wanaripotiwa kuwa waasi walioshiriki kwenye mauaji ya halaiki nchini Rwanda yaliyodumu kwa siku 100 miaka 13 iliyopita.