Kinshasa: Watu wafariki kwenye ajali ya garimoshi nchini Kongo (Kinshasa) | Habari za Ulimwengu | DW | 02.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Kinshasa: Watu wafariki kwenye ajali ya garimoshi nchini Kongo (Kinshasa)

Kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kimetangaza watu kati ya 30 na arobaini wamefariki dunia kwenye ajali ya gari moshi.

Watu wengine kadha wamejeruhiwa katika ajali hiyo

Mabehewa kadha ya gari moshi hilo la usiku yanasemekana yalipinduka.

Gari moshi hilo lilikuwa linaelekea katika mji wa Kananga ambao ni mji mkuu wa jimbo la kusini la Kasai Magharibi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com