1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA: Watu takriban 17 wauwawa

28 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBxN

Watu takriban 17 wameuwawa kwa kupigwa au kukatwakatwa na watu wanaotuhumiwa kuwa waasi wa Rwanda kwenye mkoa wa Kivu Kusini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Inaripotiwa kwamba watu wengine yapata 30 walijeruhiwa na madarzeni kadhaa wakatekwa nyara wakati waasi hao walipovivamia vijiji viwili mnamo juzi Jumamosi.