1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA: Watu 10 wauwawa kwenye ajali ya treni

14 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCSP

Watu wasiopungua kumi wameuwawa na wengine 11 kujeruhiwa kufuatia ajali mbaya ya treni ya mizigo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Ajali hiyo ilitokea jana wakati treni hiyo ilipoacha reli mjini Katanga, kusini mashariki mwa Kongo.

Samy Kayuwe, afisa wa kampuni ya kitaifa ya safari za reli, amesema abiria wote walioathiriwa ndani ya treni hiyo hawakuwa abiria halali maana sheria hairuhusu treni ya mizigo kubeba abiria.