1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kinshasa. Wagombea watakiwa kuheshimu matokeo.

15 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD2b

Ibrahim Gambari naibu katibu mkuu wa umoja wa mataifa , ametoa wito jana kwa wagombea wa kiti cha urais katika jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo , DRC kuheshimu matokeo ya uchaguzi utakaofanyika mwezi huu.

Gambari amewaambia waandishi wa habari baada ya kukutana na wagombea hao kuwa amekwenda huko ili kuwahimiza wagombea kukubali matokeo kwa maslahi ya wananchi wa Kongo.

Akikumbusha kuwa uchaguzi huo ni wa kwanza huru, katika jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo katika miongo kadha , amesema kuwa ni jukumu la wagombea kuhakikisha kuwa matumaini ya wananchi wa Kongo hayataharibiwa.

Duru ya pili ya uchaguzi ilihitajika baada ya ushindi wa Joseph Kabila katika duru ya kwanza , kuwa hautoshi kumpa madaraka moja kwa moja.