1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA: Nzanga Mobutu aachiliwa huru akiwa salama

27 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCyh

Tume ya Umoja wa Mataifa ya kulinda amani nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo imetangaza kwamba mshirika wa rais Joseph Kabila, Nzanga Mobutu, ameachiliwa huru bila madhara yoyote hii leo baada ya mapigano yaliyosababisha watu wanne kuuwawa.

Kuachiliwa huru kwa kiongozo huyo kumefanyika siku ya mwisho ya kampeni za duru ya pili ya uchaguzi wa rais nchini Kongo.

Nzanga Mobutu alikamatwa na waasi walio watiifu kwa makamu wa rais, Jean Pierre Bemba hapo jana, wakati yeye na walinzi waliokuwa na silaha walipoingia katika ofisi za kituo cha redio ya Liberty inayomilikiwa na Bemba mjini Gbadolite, kaskazini magharibi mwa Kongo.