1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kinshasa. Mtalii afariki.

8 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBkz

Wafanyakazi wa uokozi wameupata mwili wa mtalii kutoka China jana Jumamosi ambaye alianguka na kufariki katika volcano katika jamhuri ya kidemokrasi ya Congo siku ya Ijumaa.

Mtalii huyo mwanamke alianguka kiasi cha mita 140 wakati akijaribu kuchukua picha za kumbukumbu katika bwawa hilo la volcano kiasi cha mita 1,200 karibu na mlango wa volcano hiyo, mtaalamu wa mambo ya Volcano Jacques Durieux kutoka Ufaransa ameliambia shirika la habari la AFP kutoka katika eneo la Nyiragongo, ambalo volcano yake ililipuka mwaka 2002.

Mwanamke huyo kutoka Hong Kong hakutajwa jina lake. Alikuwa akisafiri pamoja na wasaidizi katika mbuga ya taifa ya Virunga wakati ajali hiyo ilipotokea.