1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA: Mapigano yazuka jamhuri ya kidemokrasia ya Congo

21 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCqr

Kumezuka mapigano makali katika jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kati ya wafuasi wa rais Joseph Kabila na mpinzani wake Jean Pierre Bemba.

Watu kiasi ya 2,000 tayari wameyatoroka mapigano na kujisalimisha katika nchi jirani ya Congo-Brazaville.

Rais Joseph Kabila alitangazwa mshindi wa uchaguzi wa mwezi uliopita na asili mia 58 ya kura. Jean Pierre Bemba alitupilia mbali matokeo hayo na kuanzisha upinzani mkubwa.