1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA: Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon ahutubia bunge la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

28 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCX9

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, aliye barani Afrika kwa ziara ya kwanza tangu aliposhika wadhifa huo, amewaambia raia wa Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo kwamba Umoja huo uko tayari kuwasaidia kukarabati nchi yao.

Ban Ki-Moon aliyekuwa akilihutubia bunge jipya la Kongo, amesema Umoja huo hauna nia ya kupunguza vikosi vyake nchini humo hivi karibuni.

Muda wa zaidi wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini humo, unapaswa kuidhinishwa na Baraza la Usalama la Umoja huo mwezi ujao ambapo wanachama wa baraza hilo wanatarajiwa kuamua endapo pana haja ya kubakisha idadi ya sasa ya wanajeshi elfu kumi na saba.

Ban Ki-Moon anatarajiwa kuzuru nchi jirani ya Kongo Brazaville na pia Ethiopia kwenye ziara yake hiyo ya Afrika.