1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA: Hali ni ya kutisha jamhuri ya kidemokrasia ya Congo

17 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCrp

Majeshi ya Umoja wa mataifa na Umoja wa Ulaya ya kulinda amani katika jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, yamatawanywa na kuwekwa katika hali ya tahadhari kufuatia kuzuka hali ya kutisha baada ya rais Joseph Kabila kutangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais. Majeshi hayo ya kimataifa yameshika doria kuepusha uwezekano wa kutokea mapigano kati ya wanajeshi na mashabiki wa rais Kabila na mpinzani wake Jean Pierre Bemba ambao waliutikisa mji mkuu wa Kinshasa mwishoni mwa wiki.

Bemba alitupilia mbali matokeo ya uchaguzi na kwamba atatumia kija njia halali kuyapinga matokeo hayo.