KINSHASA : Bemba yumkini kwenda Ureno | Habari za Ulimwengu | DW | 31.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KINSHASA : Bemba yumkini kwenda Ureno

Makamo wa rais wa zamani katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo Jean-Piere Bemba ambaye ameomba hifadhi kwenye ubalozi wa Afrika Kusini kufuatia mapigano ya hivi karibuni yumkini akaelekea Ureno mwishoni mwa juma hili kwa sababu za kimatibabu.

Duru katika ubalozi wa Ureno mjini Kinshasa zimesema kuna mambo machache ya kukamilishwa lakini wanafikiri kwamba kuondoka kwake pamoja na familia yake kunaweza kukawa mwishoni mwa juma.

Hata hivyo duru hizo zimeongeza kusema kwamba Bemba hakuomba hifadhi ya kisiasa nchini Ureno na kwamba atafanyiwa matibabu ya jeraha la mguu ambapo aliwahi kufanyiwa operesheni hapo mwezi wa Desemba mwaka jana katika hospitali ya Lisbon.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com