Kinshasa. Bemba agoma kurejea. | Habari za Ulimwengu | DW | 01.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Kinshasa. Bemba agoma kurejea.

Kiongozi wa chama cha upinzani katika jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo Jean-Pierre Bemba hatarejea nyumbani kwa hivi sasa hata kama muda wa ruhusa ya kutokuwepo kutoka katika baraza la Seneti nchini humo unamalizika usiku wa manane Jumanne.

Msemaji wake amesema kuwa Bemba , kiongozi wa waasi wakati wa vita vya mwaka 1998-2003 nchini Kongo ambaye alikuwa wa pili katika uchaguzi mkuu mwaka jana , alikwenda nchini Ureno kwa matibabu mwezi Aprili baada ya wapiganaji wake kushindwa katika mapigano ya mjini Kinshasa na majeshi ya rais Kabila.

Baraza la Seneti ambalo Bemba ni mjumbe , lilimpa likizo ya siku 60 ya kutokuwepo , likizo ambayo ilirefushwa hadi Julai 31 kutokana na ombi lake katikati ya mwezi Juni. Bemba aliahidi kurejea katika nchi hiyo ikiwa atapatiwa uhakikisho wa usalama wake.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com